My Blog List

Thursday, March 1, 2012

MAAJABU YA WATU WENYE ULEMAVU WA VIUNGO.

Zana hizi ni moja ya tamaduni zinazotumiwa  karibu na kabila zote hapa nchini lakini ikumbukwe asilimia kubwa ya wanaotengeneza zana hizi ni watu wenye ulemavu wa viungo ambao huchukua muda mwingi kukaa chini wakiwa na vifaa vyao karibu bila kuzunguka kwenda hatua zaidi ya kumi.

Mmoja wa wataalamu wa kutengeneza zana hizi maaruku Ngoma Bw.Elias Zachalia (25) na mzaliwa wa Kata ya Izimbya Wilaya ya Bukoba Vijijini Mkoa wa Kagera nchini Tanzania.

Nilipohojiana naye amesema yeye hakupata nafasi ya kusoma au kupelekwa shule kwa maana wazazi wake hawakuwa tayari kumsomesha kutokana na maumbile yake.Ikumbukwe jamii kubwa ya watanzania haikuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na ulemavu na hata wakati wa kwenda kwenye shughuli mbali mbali za kijamii mfano sherehe,ibada na mkusanyiko wowote.

Bw.Zachalia alisema kwa kipindi hicho wakati anaachwa nyubani  alikuwa akifanya utundu wa kutengeneza vitu mbali mbali kama kutengeneza vinyago vya udongo na vya nguo ambavyo alikuwa akivitoa kama zawadi ambako katika pitapita ya watu wa kitalii kupitia Kampuni ya Utalii ya KIROYELA iliona ni vema kumchukua ili kuinua kipaji chake.

Si huyo tu KIROYELA imechukua watu wengine wenye ulemavu na kwa jinsia zote hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Januari 2012 tangu 2008 waanze kuwakusanya wamefikia 45 lakini hivi sasa waliopo ni ni sita ikiwa mwama mama mmoja na wanaume ni watano.

No comments:

Post a Comment