My Blog List

Friday, March 2, 2012

UCHUMI NA MAENDELEO


WATOTO WA KIKE WAJENGEWE UWEZO WA KUMUDU MAISHA.


Hali ya sasa ya watoto wa kike hasa waishio maeneo ya vijijini kwa walio wengi wanatoka katika familia zenye kipato cha chini na asilimia kubwa wana uwezo wa kiakili kwa maana ya uwezo wa kumudu masomo ya darasani lakini wakifikia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari hapo ndipo kunakuwepo na ugumu.

Hali ya kipato cha wazazi cha kumpeleka mtoto wa kike shule inashindikana kiasi cha kumkatisha tamaa na kumfanya ajiingize kwenye vishawishi vingine na hivyo ili kuondoa tatizo hili katika  jamii yetu ya Kitanzania,kunahitajika jitihada za pamoja za Serikali,Taasisi mbali mbali na wadau wa Maendeleo wawe na dhamira ya kweli na matumizi sahihi za raslimali zilizopo.

Serikali na wadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla inabidi kuwabaini watoto wa kike ambao wako katika Mazingira hatarishi kwa sababu ya umaskini wa familia zao wameshindwa kupata haki zao za msingi na kwamba wakiwabaini wataweza kuwalipia karo na mahitaji mengineyo ya shule.

No comments:

Post a Comment